Je Unaanza Kuona Yafuatayo Yanakusumbua???
1. Kukosa kumbukumbu kama vile kusahau tarehe muhimu au matukio muhimu
2. Kupata shida katika kufanya mambo ya kawaida, kama kukumbuka sheria za mchezo unaoupenda au kuendesha gari kuelekea sehemu unayoifahamu vizuri
3. Kupata shida katika mazungumzo na wenzako au katika kuandika, kwa mfano kupata shida katika kukumbuka maneno sahihi au majina ya watu na sehemu mbalimbali
4. Kupoteza mwelekeo wa muda na mahali, kama kusahau sehemu ulipo, kutojua msimu wa mwaka, tarehe, na muda uliotumia katika shughuli
5. Kupungua uwezo wa kutoa maamuzi kama kukosa usafi, kushindwa kutoa maamuzi ya pesa n.k
6. Matatizo katika kuona kama matatizo katika kusoma au kukadiria umbali
7. Kupungua kwa uwezo wa kutatua matatizo na kuweka mikakati kama ufuatiliaji wa bili mbalimbali au kukumbuka mapishi
8. Kupoteza vitu kila wakati au kusahau villipowekwa
Ukiona baadhi ya mambo yaliyoorodheshwa hapo juu yanakuhusu, ujue upo hatarini kuugua ugonjwa wa Alzheimer’s.
.
.
UGONJWA WA ALZHEIMER'S NI NINI ???
Ni dosari inayoendelea kuongezeka taratibu ambapo husababisha seli za ubongo kuharibika na kufa.
Ugonjwa wa alzheimer’s ndiyo chanzo kikubwa cha tatizo liitwalo dimentia – kuendelea kupoteza uwezo wa kufikiri, tabia katika jamii na linalomfanya mtu ashindwe kumudu shughuli zake yeye peke yake.
.
.
ATHARI ZA MTU MWENYE ALZHEIMER'S :
Kurudiarudia maswali au maneno
Kusahau mazungumzo, ahadi au matukio, na asikumbuke tena baadaye
Kila wakati kupoteza vitu vyake, mara nyingi akiwa anaviweka sehemu ambazo hazitegemewi
Kuanza kupotea maeneo aliyoyazoea
Hatimaye kusahau majina ya watu wa familia yake na vitu vya kila siku
Shida katika kupata maneno sahihi kutambulisha vitu, kuelezea mawazo yake au kushiriki kwenye mazungumzo, kufikiri Na Kuchambua
Ugonjwa wa alzheimer’s humfanya mtu ashindwe kutuliza mawazo kwenye kitu kimoja na kufikiri, hasa kuhusu vitu vya kinadharia kama namba.
.
.
MADHARA ANAYOWEZA KUYAPATA MGONJWA:
• Mfadhaiko
• Kutopenda vitu/ kutokuwa na hisia
• Kujitoa kwenye mambo ya kijamii
• Kubadilikabadilika kwa hisia kwa ghafla
• Kutopenda wenzake
• Hasira
• Kubadili ratiba ya kupata usingizi
• Kuzurura
• Kushindwa kujizuia vishawishi
• Kuwa na imani za uwongo, kama kuamini kuwa ameibiwa
.
.
Chanzo Kamili Cha Ugonjwa huu bado hakijaeleweka, lakini unapofika kilele chake huwa ni matatizo katika protini za ubongo ambazo zinashindwa kufanya kazi vizuri, kuvuruga utendaji wa seli za ubongo (neurons) na kutoa sumu za aina mbalimbali. Neurons huharibiwa, zinapoteza mawasiliano na kisha kufa
Uharibifu mara nyingi huanza kwenye sehemu ya ubongo inayohusiana na kumbukumbu
Ukosefu huu wa neurons kisha husambaa kwenye maeneo mengine ya ubongo. Ugonjwa unapokuwa mkubwa, ubongo huwa umesinyaa kwa kiasi kikubwa.
.
.
VIHATARISHI VYA ALZHEIMER'S :
1.Umri :
Kihatarishi kikubwa zaidi kuliko vyote cha ugonjwa wa alzheimer’s ni umri mkubwa
Kadiri kundi la jamii linavyozidi kuwa na umri mkubwa, ndivyo watu wenye tatizo hili wanavyozidi kuongezeka. Asilimia 15 ya watu wanaozidi miaka 65 na asilimia 50 ya wale wanaozidi miaka 85, wana tatizo la alzheimer’s.
.
.
2.Historia Ya Familia :
Uwezekano wa kupatwa na ugonjwa huu unachangiwa pia na vinasaba. Watu wengi huupata ugonjwa huu umri wao unapofikia miaka 70
Lakini, pungufu kidogo ya asilimia 10 ya watu hupata ugonjwa huu wakiwa na umri wa maika kati ya 40-50. Yapata nusu ya watu hawa hupata ugonjwa huu kwa sababu za kiurithi.
.
.
3.Jinsia :
Tafiti zimeonyesha kuwa wanawake wanaupata ugonjwa huu zaidi ya wanaume
Ni ukweli kuwa wanawake wanaishi maisha marefu zaidi ya wanaume, lakini pekee hautoshi kuelezea sababu ya kuzidi kwa ugonjwa huu kwa wanawake
.
.
4.Kuumia :
Watu waliopata maumivu makali ya kichwani (emotional or physical damage) wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kuupata ugonjwa huu
Watu wenye tatizo hili la kukosa kumbukumbu hupatwa na mchanganyiko wa hisia – kuchanganyikiwa, kukata tamaa, hasira, woga, uchungu na mfadhaiko
Kama unamhudumia mtu wa namna hii unaweza kumsaidia zaidi kwa kuwa msikivu kwa shida zake, kwa kumhakikishia kuwa bado anaweza kuishi maisha ya kawaida, kumpa misaada na kufanya uwezavyo kumrudishia hali ya kujiamini na kuheshimiwa
Mazingira tulivu yanaweza kumsaidia matatizo yake ya kitabia. Mazingira mapya, kelele, mikusanyiko ya watu, kumharakisha kukumbuka vitu, au kumtaka afanye shughuli zinazohitaji fikra vinaweza kumfanya apate wasiwasi
Na mtu wa tatizo hili akipatwa na wasiwasi, uwezo wake wa kufikiri hupungua zaidi.
.
Tambua Mmea Mzuri Kwa Ugonjwa Huu
GINKGO
Mmea wa ginkgo una tabia nyingi za tiba. Watu wengi huliita ginkgo jani la ubongo “brain herb”, ambalo limeonyesha kuboresha utendaji kazi wa ubongo
Ubongo hutumia asilimia 20 ya oksijeni ya mwili. Kwa sababu ginkgo husaidia mzunguko wa damu katika ubongo, kwa kupeleka oksijeni kwa haraka zaidi na kiufanisi
Faida ni nyingi, kama kutoa tiba ya mfadhaiko (depression) na kuongeza kumbukumbu, matendo hisia (Reflexes), na ufanyaji kazi wa ubongo kwa ujumla
Utafiti wa karibuni umeonyesha kuwa inaweza kupunguza madhara ya dementia kwa wagonjwa wenye Alzheimer’s, na kufungua njia ya tiba ya aina mpya ya ugonjwa huu ulioenea na usioeleweka vizuri
Pia Vitamin E. Vitamin E inaweza kuzuia ukuaji wa ugonjwa wa alzheimer’s
Endapo utahitaji kirutubisho chenye mmea huo wa gingko ambayo inafanya vizuri kwa wagonjwa hawa wa kupoteza kumbukumbu PIGA SIMU au TUMA UJUMBE kwenda +255716778844 SASA HIVI
JE UNGEPENDA KUANZA MATIBABU YA CHANGAMOTO HII ????
BONYEZA NENO WHATSAPP HAPO CHINI ILI UWEZE KUSAIDIWA TIBA
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
0 Comments