Games

6/recent/ticker-posts

Ujue Ugonjwa Wa KIHARUSI (STROKE) Na Matibabu Yake...

Unajua Inakuwaje Mtu Anapata Ugonjwa Wa Kiharusi (Stroke)…???

Kiharusi Maana Yake Nini ????
.
.
Kiharusi ni ugonjwa wa dharura na hatari ambao hutokea pale seli za ubongo zinapokufa kwa kukosa hewa ya oksijeni na chakula kutokana na kuziba au kupasuka kwa mishipa ya damu kwenye ubongo.

Aina Za Kiharusi:

Kuna aina kuu mbili za Kiharusi

1. Kiharusi kinachotokana na kuziba kwa mishipa ya damu ya damu ya ubongo

2. Kiharusi kinachotokana na kupasuka kwa mishipa ya damu ya ubongo
.
.


Ukubwa Wa Tatizo La Kiharusi:

1. Kiharusi ni muuaji namba 2 : Kwa mwaka 2015 kulingana na ripoti maalumu ya Shirika la Afya duniani WHO kuhusu sababu za vifo ilionesha kiharusi kinashika nafasi ya pili kati ya magonjwa yote kwa kusababisha vifo vingi.

2. Kiharusi husababisha ulemavu kwa wengi : Kiharusi kinashika nafasi ya tatu kati ya visababishi vya ulemavu duniani. Waathirika wengi huishia kuwa walemavu 
.
.
Dalili za kiharusi:

1.Ganzi:

Mtu anayepata kiharusi hupata ganzi inayoanza ghafla na mara nyingi huathiri upande mmoja wa mwili. Mfano: Upande mmoja wa uso kufa ganzi na kushindwa kuongea vizuri au kutabasamu
.
.
2.Kupata Shida Ya Kuongea:

Mgonjwa wa kiharusi hushindwa kuongea vizuri, utoaji wa maneno huwa sio wa kawaida

Mfano: Mgonjwa kushindwa kumaliza sentensi au kuongea kama amelewa sana

Pia hali hii huweza kuambatana na kutoka mate(udenda) kwa wingi mdomoni
.
.
3.Kushindwa Kuona Vizuri:

Mgonjwa wa kiharusi anaweza kushindwa kuona, hali hii hutokea ghafla. Inaweza kuhusisha jicho moja au macho yote mawili
.
.
4.Kupoteza Fahamu:

Pia mgonjwa anaweza kupoteza fahamu au kupata degedege
.
.
5.Kushindwa Kuzuia Haja:

Mgonjwa anaweza kushindwa kuzuia haja kubwa au ndogo au vyote viwili
.
.
Vinavyochangia Mtu Kupata Kiharusi:
1. Ugonjwa wa Shinikizo kubwa la damu (presha)
2. Uvutaji sigara
3. Ugonjwa wa kisukari
4. Magonjwa ya moyo hasa ugonjwa wa mtetemo wa moyo (atrial fibrillation)
5. Tatizo la mafuta mengi kwenye damu (Lehemu au cholesterol)
6. Uzito uliopitiliza
7. Unywaji wa pombe uliokithiri
8. Kutokufanya mazoezi
.
.
Gundua kiharusi haraka uokoe maishayako, ya mpendwa, ndugu au jamaa yako

Kiharusi ni tatizo la dharura linaloweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo kifo au ulemavu kama mtu asipopata matibabu mapema.
  
Hivyo ni vyema kila mtu akafahamu dalili za kiharusi ili iwe rahisi kuzitambua. na kuchukua hatua mapema.

Ili kurahisha kumbukumbu za dalili za kiharusi kifupisho FAST (Face Arm Speech Time) hutumika kama ifuatavyo:

-Face (Uso ):

Angalia kama upande mmoja wa uso uko tofauti na mwingine. Mwambie mgonjwa. anyanyue kope au akunje ndita au atabasamu. Upande ulioathrika utashindwa kufanya hivyo.
.
.
-Arm (Mkono):

Mwambie mgonjwa anyanyue mikono juu kwa mbele au juu mara nyingi mkono wa upande ulioathirika hushindwa kunyanyuka au hudondoka unaporudishwa chini.
.
.
-Speech (Uongeaji):

Mwambie mgonjwa atamke jina lake, mtu mwenye kiharusi hushindwa kuongea, au huongea kama. mlevi au hupata shida kutafuta maneno kama mtu aliyepoteza kumbukumbu
.
.
-Time (Muda):

Muda ni mali, chukua maamuzi ya kutafuta msaada wa kitabibu haraka maana kadri unavyochelewa ndio kiharusi kinaharibu sehemu muhimu za ubongo
.
.
Ushauri:

Usisubiri mpaka upate ugonjwa huu, njia bora kabisa ni kuhakikisha mishipa yako ya damu inakuwa salama kabisa.

Changamoto watu wenye sukari nyingi kwenye damu au wenye shinikizo la damu mishipa yao inakua imeathirika hivyo ni rahisi kupata kiharusi
  
Tumekuandalia virutubisho ambavyo vitasaidia kuhakikisha kwamba ubongo unapata hewa safi,chakula na pia damu inatirirka vizuri kwenye ubongo na kwenye mishipa yote lakini kubwa zaidi inaenda kurekebisha na kutibu mishipa yote ya damu iliyokuwa imeharibika u kusinyaa.
  
Jikinge sasa kabla hujapatwa na tatizo maana gharama za tiba zitakuwa ghali sana.Kinga ni bora kuliko tiba. Na hata ambao tayari wana tatizo tunawasaidia.
  
Wenye matumizi makubwa ya ubongo kama vile wanafunzi, wafanyakazi wa mahesabu,wanaotumia computer nk wote wanahitaji bidhaa hizi

JE UNGEPENDA KUANZA MATIBABU YA CHANGAMOTO HII?


                                           














Post a Comment

0 Comments