Lijue Suluhisho La Maumivu Ya Viungo,Kiuno,Shingo Na Mgongo,Miguu Kuwaka Moto,Kukakamaa Kwa Misuli
.
Hali hii imekua changamoto kwa wazee,wanamichezo,wenye uzito mkubwa wanyanyua vyuma na wana gym.
Hii ni kwasababu umri unavyozidi kwenda mwili unashindwa kuzalisha ute ute katika viungio vya mifupa,na hivyo kupelekea misuguano ya mifupa,ambapo husababisha maumivu makali sana na kupelekea mtu kushindwa Kukaa,Kuinuka,Kukimbia au Kutembea Kabisa!!
.
.
Mara Nyingi Ugonjwa Huu Huitwa ARTHRITIS,Unasababishwa na hitilafu yoyote katika sehemu hizo za maungio ya mifupa.
Inaweza kuwa cartilage inalika,upungufu wa synovial fluid(Maji Maji Katika Maungio),maambukizi ya vijidudu katika moja ya maeneo hayo au mchanganyiko wa matatizo Mbali Mbali,Ikiwemo Uzito mkubwa.
Tabia kuu ya magonjwa haya ni maumivu kwenye maungio ya mifupa (joints) ambayo ni endelevu na ambayo hutokea eneo hilo hilo moja.
Chanzo Cha Arthritis Ni Nini...?
Ili Upate Kuelewa Vyema Chanzo cha ugonjwa huu,hebu kwanza tutazame muundo wa joint au sehemu mifupa miwili inapokutana(Maungio).
Mfano Goti ambapo mifupa miwili mmoja wa paja na mwingine wa mguu vinapokutana:
Maungio ya mifupa-Ligaments;
Ndicho kitu kinachoshikilia mifupa hii miwili pamoja,hii ni kama utepe wa plastiki au mpira unaonyumbuka uliozunguka eneo hilo kwa nje,ukikunja goti inanyumbuka na ukinyoosha mguu inarudi.
Cartilage;Huu ni utando unafunika eneo ambalo mifupa hugusana ili kuzuia mifupa hii isisuguane moja kwa moja,Utando huu ambao kwa kiswahili tunauita gegedu huyawezesha maungio hayo kufanya kazi kiulaini pasipo kusababisha maumivu.
Capsule;Hiki ni kitu kinachofunika maungio haya kikizunguka pande zote,ndani ya mfuko huu wa capsule kuna synovial fluid ambayo huzalishwa na synovial membrane.
Synovial fluid ni ute ute wa kulainisha sehemu hiyo ya maungio na synovial membrane ni utando ulio kwenye kuta za ndani za capsule.
Kama nilivyoeleza hapo juu,kuwa kuna aina zaidi ya 100 za ugonjwa huu wa joints au arthritis.
Katika mada yetu ya leo tutatazama aina mbili za ugonjwa huu,tukielezea chanzo cha kila aina....
1. Osteoarthritis.
Hii ni aina ya arthritis inayosumbua watu wengi zaidi kuliko aina nyingine zote...
Ugonjwa huu huwapata zaidi watu wenye umri mkubwa,Osteoarthritis hutokea pale cartilage inapopoteza uwezo wake wa kubonyea na kuwa ngumu hivyo kuharibika haraka.
Cartilage ni kiungo cha kuhimili migandamizo ya ghafla (shock absorber),Cartilage hii inapopoteza ubora wake,tendons na ligaments huvutika na kusababisha maumivu.
Hali ya uharibifu huu wa cartilage ikiendelea,mwishowe mifupa huanza kusuguana moja kwa moja na ndipo mgonjwa atakapoanza kupata maumivu makali sana sana.
Athari za ugonjwa huanza taratibu na kuongezeka zaidi,Mgonjwa ataanza kupata maumivu kwenye joint baada ya kufanya shuguli fulani au baada ya mapumziko ya muda mrefu. Joints zitaanza kukaza siku hadi siku,Hasa wakati wa asubuhi unapotaka kuanza shughuli zako za kawaida.
Na siku zinavyosogea ndivyo utakavyoona ni vigumu zaidi kukitumia kiungo chako,Mara nyingine utaona uvimbe kwenye joint.
Osteoarthritis hushambulia zaidi nyonga,mikono,magoti na uti wa mgongo.
2. Rheumatoid arthritis.
Ugonjwa huu hutokea pale mfumo wa kinga ya mwili unapopungua,viungo huanza kushambuliwa, ikiwa ni pamoja na synovial membrane (synovium) na kusababisha uvimbe na maumivu.
Hali hii isipodhibitiwa,huweza kusababisha ulemavu. Ugonjwa huu unaweza pia kushambulia macho,ngozi,mapafu,midomo,damu na mishipa ya damu. Huu ni ugonjwa ambao zaidi ni wa wanawake na huwatokea zaidi wawapo kati ya umri wa miaka 40 hadi 60.
Mgonjwa atasikia maumivu na kuona uvimbe kwenye joints za pande zote za mwili;
Yaani kama ni magoti,yote mawili yatashambuliwa na Viungo vinavyoshambuliwa zaidi ni vidole,viwiko vya mikono na miguu.
Athari zake huonekana zaidi asubuhi unapoamka na maumivu yanaweza kudumu kwa muda wa hadi nusu saa.
Muathirika wa ugonjwa huu hujisikia mchovu muda wote, hukosa hamu ya kula na hupungua uzito,Ugonjwa huu huweza kukua zaidi na Kusababisha matatizo katika viungo vyote vya mwili.
Matatizo yanayoweza kujitokeza ugonjwa ukikua ni kama yafuatayo:
a) Macho kuwa na ukavu,maumivu,wekundu,kutopenda mwanga na kutoona vizuri
b) Midomo,Ukavu au kukauka kwa lips za midomo,maumivu na maambukizi ya fizi
c) Ngozi,Vijinundu chini ya ngozi kwenye maeneo yenye mifupa
d) Mapafu,Kushindwa kupumua vizuri
e) Mishipa Ya Damu,Uharibifu wa mishipa ya damu
f) Damu,Upungufu wa chembechembe nyekundu za damu
.
Changamoto kubwa ya matatizo ya joints na mifupa huwapata wana michezo,wanyanyua vyuma(body builder),watu wanaofanya kazi ngumu,mafundi magari,wabeba mizigo na madereva wa masafa marefu na wafanyakazi wa mahofisini wanao fanya kazi za kukaa zaidi.
SULUHISHO KWA MGONJWA MWENYE TATIZO LA JOINTS NA KUJIKINGA NA TATIZO LA JOINTS
Hakuna Ugonjwa usio na suluhisho kama ukiuwahi mapema,japo pia ukichelewa ina kuwa ni mbaya zaidi ila suluhisho halikosekani kabisaa!!
Na Suluhisho pekee la Tatizo La Joints ni kutumia Virutubisho(Food Supplements),kwa mwenye tatizo ama kwa wanaofanya mazoezi ili kuongeza huo ute ute kwa lengo la kuzuia misuguano ya joints
Na hapa tumekuandalia package nzuri sana kwa matatizo yote ya mifupa na maungio. Endapo una tatizo hili au ndugu yako basi usisite kuwasiliana nasi ili tuweze kukusaidia na kuanza tiba yako leo
JE UNGEPENDA KUANZA MATIBABU YA CHANGAMOTO HII
0 Comments