Hebu Jifanyie Uchunguzi Wa Matiti Yako Ukiwa Nyumbani Kwa Njia Hizi HAPA...
NDIO jifanyie uchunguzi maana siku hizi saratani ya matiti imeshika kasi sana, waswahili wanasema bora nusu shari kuliko shari kamili...
📣Endapo utahisi kitu tofauti katika titi lako kwa kuona baadhi ya dalili ambazo nitaziainisha hapa chini basi haina budi kuwahi hospitali kwa uchunguzi zaidi...
📣Kati ya wanawake 7 , mmoja hugundulika ana saratani ya titi
📣Watu wengi hugundulika na saratani ya titi wakiwa na umri wa zaidi ya miaka 50, lakini hata vijana wanapatwa na saratani hii ya saratani
🔊Ni kwa uchache sana kuna wanaume ambao pia huugua saratani ya titi
🔊Kuna chance kubwa kwa mtu mwenye saratani ya titi kupona endapo atagundulika mapema na saratani yake ikiwa kwenye hatua za awali
🔊Angalia matiti yako mara kwa mara kama kuna mabadiliko yoyote
🔊Nenda kaonane na daktari wako ikiwa una mabadiliko yoyote au dalili ambayo sio ya kawaida.Fanya hivi hata kama ulifanya vipimo vya xray ya matiti hivi karibuni ambayo ilikuwa ya kawaida
Dalili Kuu Ya saratani Ya Titi Ni Uvimbe(buja) Ndani Ya Titi
Japo vimbe nyingi(buja) sio saratani yaani kati ya vimbe 10 basi 9 sio saratani lakini ni muhimu sana uonapo dalili hiyo ufike hospitali kwa uchunguzi maalum kutoka kwa daktari wako
Kitu kingine ni kwamba sio kila maumivu ya titi ni SARATANI....HAPANA
Baadhi Ya Dalili Za Saratani Ya Matiti
1.Uvimbe mpya au eneo la tishu mnene katika aidha titi
2.Mabadiliko ya ukubwa au umbo la matiti moja au yote mawili
3.Kutokwa na damu kutoka kwa chuchu zako zozote
4.Uvimbe au uvimbe katika mojawapo ya makwapa yako
5.Kubonyea kwa ngozi ya matiti yako
6.Upele kwenye au karibu na chuchu yako
7.Mabadiliko katika jinsi chuchu yako inavyoonekana, kama vile kuzama kwenye titi lako
.
.
Mazingira Hatarishi Yanayoongeza Uwezekano wa Kupata Saratani ya Matiti.
Kuna tabia na mazingira yanayoongeza uwezekano wa kupata saratani ya matiti. Lakini siyo kwamba sababu moja pekee inaweza kupelekea upate saratani
Baadhi ya Tabia hatarishi zinaweza kuwa ngumu kuepukika kama historia ya ugonjwa kutoka kwenye familia. Mazingira mengine hatarishi ni :
🔔Umri:
wanawake wenye umri zaidi ya miaka 55 wapo kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya titi
🔔Unywaji Wa Pombe:
Wanawake wapo kwenye hatari zaidi mara 100 kuugua saratani ya titi ukilinganisha na wanaume
🔔Kuvunja Ungo Mapema:
Wanawake wanaovunja ungo kabla ya kutimiza miaka 12 wapo kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ukilinganisha na wengine
🔔Kuanza Kujifungua Katika Umri Mkubwa Hasa Kuanzia Miaka 35
🔔Tiba za homoni (hormone therapy)
Wanawake waliopo kwenye tiba ya homoni za kuchelewesha kukoma hedhi wanaongeza hatari ya kupata saratani ya matiti
🔔Kuchelewa kukoma hedhi: kuanzia miaka 55 na kuendelea
🔔Kutozaa kabisa
🔔Waliowahi kupata saratani ya matiti kipindi cha nyuma
🔔Matumizi ya vidonge vya kupanga uzazi kwa muda mrefu
🔔Urithi : Wengine hupata hii kwa kurithi katika ukoo
.
.
Dalili za Saratani Ya Matiti
Saratani inapoanza haioneshi dalili zozote. Mgonjwa anaweza kutambua uwepo wa uvimbe wa saratani kwa kufuata maelekezo ambayo tutatoa hapa chini.
Kila aina ya saratani inaweza kusababisha dalili mbalimbali
Dalili Zifuatazo Ni Zile Zinazoingiliana:
🔰Uwepo wa tishu ngumu ambazo ni tofauti na tishu zingine
🔰Kupata maumivu kwenye titi
🔰Rangi ya titi kubadilika na kupata wekundu
🔰Uwepo wa mbonyeo kwenye titi
🔰Chuchu kuingia ndani (nipple retraction)
🔰Kuvimba kwa titi
🔰Kutokwa na majimaji yasiyo maziwa kwenye matiti
🔰Kutokwa na damu wenye chuchu za titi
🔰Kupata mabadiliko ya umbo la titi kusiko kawaida
🔰Kuhisi uvimbe au nundu kwenye titi
Angalizo: Siyo kwamba ukiona dalili mojawapo kati ya hizi ndio uhakikisho kwamba una saratani ya matiti hapana. Unapopata dalili hizi hakikisha unaenda hospitali kufanya vipimo mapema ili kupata uhakika juu ya tatizo.
Jinsi ya Kugundua uwepo wa Saratani kwenye Titi kwa Kutumia Mkono...
👇👇👇
Jinsi Ya Kuchunguza Matiti Yako.....
Hatua Ya 1
Angalia kama kuna utofauti au mabadiliko yoyote katika matiti yako . Simama na uangalie kwenye kioo chako huku mikono yako ikiwa kwenye kiuno na mabega yako sawa sawa
Hatua Ya 2
Inua mikono yako na uangalie mabadiliko katika eneo la muonekano wa matiti yako. Angalia kama chuchu zina mabadiliko yoyote au kutokwa na majimaji au chochote katika chuchu hizo
Hatua Ya 3
Lala chali . Tumia mkono wako wa kulia kugusa titi lako la kushoto na kisha mkono wako wa kushoto kugusa titi lako la kulia.Weka vidole vyako pamoja. Kwa mwendo wa mviringo yaani unakuwa kama unaandika sifuri kwa hivyo vidole vyako kuzunguka titi lako kutoka juu hadi chini na upande hadi upande. Sogeza mkono wako kutoka kwenye mfupa wa shingo hadi juu ya fumbatio lako, na kutoka kwenye kwapa hadi kwenye mpasuko wako
Inaweza kuwa ni rahisi kuhisi matiti yako wakati ngozi yako ikiwa imeloana na maji na kuteleza, kwa hivyo unaweza kufanya zoezi hili wakati wa kuoga , utakuwa unazungusha kwenye titi lako au unabonyeza titi lako moja moja, pole pole na kuangalia kama utahisi ugumu wowote eneo hilo la titi
.
.
Jitahidi kujiepusha na mambo yafuatayo ili kujiweka mbali na saratani hii ya matiti japo mpaka sasa chanzo sahihi hakijajulikana
.
.
🔰Jitahidi uwe unafanya vipimo mara kwa mara
🔰Fanya mazoezi kila siku kwa dakika 30-60
🔰Punguza tiba za homoni
🔰Epuka matumizi ya sigara na tumbaku
📣Mpaka kufikia hapo najua umefaidikia na elimu hii na hiyo ndio furaha yangu , ulichojifunza hapa usikae nacho peke yako bali nenda kawafundishe wanawake wenzako ili tuweze kusaidia wengi
📣Kwa wale ambao tayari wameshaanza kuona dalili mbaya basi naomba kwamba WAHI hospitali kwa ajili ya vipimo vya kina kujua kama tatizo hilo unalo au huna na endapo utakutwa una hilo tatizo basi utaanzishiwa matibabu haraka kabla tatizo halijakua kubwa kwa kusambaa
📣Lakini pia kama umegundulika na hili tatizo basi usisite kuwasiliana nami ili niweze kukusaidia kwa ushauri ambao najua unaweza kukusaidia
📣Na pia ukiwa haujapata shida hii bado pia unaweza kunitafuta ili niweze kukusaidia nini cha kufanya ili uepukane na shida hizi .. Kumbuka ni bora kuepuka kuliko kutibu maaana gharama huwa inakuwa kubwa sana kwa tatizo lolote lile la ki afya
✉Wasiliana nasi kwa ushauri au tiba kwa namba hiyo hapo chini
📞Simu/ Whatsapp : +255 716 778 844
0 Comments