Je Unajua Kwanini Unapata Hedhi Nyeusi???
Wanawake wengi wanaanza hedhi baada ya kuvunja ungo miaka 12 na 13, ikiwa hakuna tatizo lolote la kiafya. Hedhi ni damu inayotoka kila mwezi baada ya ukuta wa kizazi kubomoka, endapo mimba haikutungwa.
Rangi na mwonekano wa hedhi yako ni kiashiria kikubwa kuhusu mwenendo wa afya yako ya uzazi.
Mabadiliko Ya Rangi Ya Hedhi
Rangi ya hedhi yako inaweza kubadilika kutoka kwenye nyekundu ya kungaa, chungwa, brown na pia nyeusi.
Ni muhimu kutambua kwamba hedhi nyeusi, siyo kwamba inakuwa nyeusi hasa hapana. Ni ile hali ya weusi usiokolea kama vile damu ilopigwa na upepo ikaganda.
Sometime hedhi nyeusi yaweza kuashiria changamoto fulani ya kiafya na ndio maana tumeandika makala hii ujifunze.
Chanzo Cha Hedhi Nyeusi
Damu nyeusi ya period inachukua muda mrefu sana kutoka nje ya kizazi, na hivyo kupitiwa na hewa. Kitendo huitwa oxidation, yani damu kuchanganyika na hewa na kuifanya iwe nyeusi au ya brown, sawa na rangi ya kahawa.
Hedhi nyeusi na na kutokwa uchafu ukeni mara nyingi siyo ishu kubwa ya kukuletea mawazo. Uke unajisafisha kila siku na hedhi yaweza kutokea ukapata nyeusi mara chache. Pamoja na hivyo unatakiwa kufuatilia afya yako na aina za uchafu unaotoka ukeni.
Sababu 8 Zinazofanya Upate Hedhi Nyeusi
1.Hedhi nyeusi kuashiria mwanzo au mwisho wa hedhi
Spidi ya kutoka damu inakuwaga ndogo sana mwanzoni na mwishoni mwa hedhi. Hedhi inavyochelewa zaidi kutoka ndipo uwezekano ni mkubwa ikapitiwa na hewa ya oksijeni na kuwa nyeusi.
2.Kuna Kitu kimekwama ukeni
Hedhi nyeusi muda mwingine inaweza kuwa kiashiria cha kitu ukeni kimekwama, vitu hivi ni kama condom, kitanzi, sex toy, sponge na tampon. Damu hii isipotoka inafanya uke kuvimba kwa ndani na kupelekea maambukizi.
Dalili hizi zinaashiria kwamba tayari umepata maambukizi ukeni na kwenye kizazi
👉Kutokwa uchafu unaonuka sana ukeni
👉Muwasho maeneo ya uke
👉Homa
👉Maumivu wakati wa kukojoa
👉Kuvimba na vipele ukeni
👉Maumivu ya tumbo chini ya kitovu na nyonga
Kama utagundua kwamba hedhi yako ni nyeusi na inaambatana na dalili mojawapo kati ya hizo juu, jua kuna kitu ndani kimekwama, jichunguze
3.Mabaki ya hedhi iliyopita
Hedhi inapokwama kutoka nje ya uke, inabaki na kugandana ndani na hivyo kubadilika kuwa nyeusi.
Maumbile ya uke yanaweza kupelekea hali hii, mfano wanawake bikira wanakuwa na utando ukeni. Utando huu unaweza kuzuia utokaji mzuri wa hedhi na kupeleke damu kuwa nyeusi.
Mara chache tatizo hili laweza kuwa kubwa zaidi na kupelekea ukose hedhi. Muone daktari endapo utakosa hedhi zaidi ya siku 40 na hauna mimba.
4.Uwezekano wa saratani ya mlango wa kizazi
Japo inatokea mara chache sana, lakini endapo unapata damu nyeusi ya hedhi, inayoambatana na kutokwa damu baada ya tendo au katikati ya mzunguko inaweza kuashiria saratani ya shingo ya kizazi.
Saratani ya shingo ya kizazi mwanzoni huwa haioneshi dalili. Pale ikifikia stage mbaya ndipo utaanza kuona dalili kama uchafu mwingi, wenye damu na unaonuka ukeni.
Dalili zingine ni pamoja na...
👉Kuishiwa nguvu
👉Hedhi kutoka zaidi ya siku 7
👉Maumivu wakati wa tendo
👉Uzito kushuka kupita kiasi
👉Maumivu ya nyonga
👉Kuvimba miguu
👉Kushindwa kukojoa vizuri
👉Kushindwa kunya vizuri
5.Hedhi nyeusi baada ya kujifungua
Baada ya kujifungua inachukua week 6 mpaka nane kwa mama kupata damu ya kwanza. Lakini kabla ya hapo mama hutokwa na damu tangu siku ya kuzaa, na damu hii kitaalamu huitwa lochia.
Damu hii ya lochia huaanza kutoka nyingi siku za mwanzo, na badae kupungua sana. Mwanzoni damu yaweza kupitiwa na hewa ya oksijeni na kawa nyeusi.
Siku kadhaa mbele damu hii itaanza kuwa nyepesi na ykekundu au ya njano kabla ya kustope kabisa. Muone daktari endapo damu yako baada ya kujifungua inaambatana na harufu mbaya siku chache baada ya kuzaa.
6.Mimba kuharibika
Mimba nyingi zinaharbika ndani ya wiki 20 za mwanzo. Wataalamu wanasema asilimia 10 ya mimba zinazotungwa hutoka mapema kabla ya muda wa kujifungua.
Baadhi ya wanawake wanachanganya hedhi na mimba iliyoharika. Mimba inapoharbika na damu zikachelewa kutoka, yaweza kupelekea damu nyeusi ya mabonge.
Unachotakuwa ni kufatilia kama utavusha hedhi kwa wiki moja na ulifanya sex, nunua UPT upime mkojo kujua kama mimba imo au uende hospitali wakupime maana wao ndio wana utaalam zaidi
7.Ukuta wa kizazi unabomoka baada ya mimba kutunga
Sometime waweza kuchanganya damu ya mimba kutungwa na hedhi. Mimba inapojishikiza kwenye ukuta wa kizazi, inapelekea eneo husika kubomoka a damu kutoka. Japo ni mara chache sana inatokea lakini inawezekana.
Damu hii ya mimba kutungwa inatokea siku 10 mpaka 14 baada ya yai lililorutubishwa kujishikiza kwenye kizazi. Damu huisha ndani ya siku chache na mara nyingi inakuwaga nyepesi, na yaweza kuwa nyeusi kwasababu inachelewa sana kutoka ukeni.
8.Hedhi nyeusi na magonjwa ya zinaa
Hedhi nyeusi ina uhusiano na maambukizi ya zinaa kama kisonono na chlamydia
Dalili zingine za magonjwa ya zinaa ni pamoja na..
👉Uchafu ukeni unaonuka
👉Kuungua wakati wa kukojoa
👉Maumivu wakati wa tendo
👉Kuhisi mgandamizo eneo la nyonga
👉Muwasho ukeni
👉Kupata damu katikati ya mzunguko
Magonjwa ya zinaa kama yasipotibiwa mapema yanaweza kupelekea PID, ambapo ni maambukizi kwenye njia ya uzazi. PID inaweza kuathiri via vya uzazi ikiwemo mirija na kupelekea ushindwe kushika mimba nyingine mapema.
Ugonjwa huu wa P.I.D umekua ni miongoni ya magonjwa yanayowatesa sana wanawake na hata wengine kupatwa na ugumba au saratani ya shingo ya kizazi isipotibiwa mapema
👉Mwisho kabisa damu nyeusi yaweza kuashiria uwepo wa changamoto kwenye kizazi kama uvimbe yaani fibroids na mimba kutunga nje ya kizazi.
Matibabu Kwa Changamoto Ya Hedhi Nyeusi
Matibabu ya tatizo yanategemea na chanzo, hakikisha unaenda hospital endapo hujui nini kimepelekea utokwe na damu nyeusi. Tiba zitakuwa kwenye mgawanyo huu
💢1.Kama kuna kifaa kimekwama ndani ya uke, daktari atakuchunguza na kukitoa haraka.
💢2.Magonjwa ya zinaa mara nyingi yanatibika kwa antibiotics.Hakikisha unafatilia matibabu yote mpaka unamaliza kwani usipomaliza dawa mwili unakuwa sugu.
💢3.Kama utavusha hedhi zaidi ya wiki mbili, muone daktari. Unaweza kuwa na mimba ama uchafu umeganda ukeni
💢4.Saratani ya shingo ya kizazi inatibiwa kwa muunganiko wa tiba ikiwemo chemotherapy, ,mionzi na upasuaji kulingana na ukubwa wa tatizo. Hakikisha unafanya vipimo vya mlango wa kizazi kila mwaka kujua kama kuna vihatarishi.
Lini Unatakiwa Kumwona Daktari?
Kama unapata damu nyeusi wakati wa ujauzito au baada ya kujifungua, au baada ya kukoma hedhi, ni muhimu kumwona daktari haraka. Yaweza kuashiria shida kubwa
NB: Tumekuwa tunasaidia wanawake wengi wenye shida hii na shida zingine kwa kutumia FEMALE PACKAGE ambayo mbali na kutibia lakini inasaidia kukulinda dhidi ya maambukizi, kuweka homoni sawa, kusaidia watu wanaotaka kudaka ujauzito, kuondoa uchafu na harufu mbalimbali ukeni na pia kukulinda na saratani ya shingo ya kizazi
Endapo unahitaji FEMALE PACKAGE au ushauri wa afya basi usisite kuwasiliana nasi kwa :
Simu/whatsapp: +255716778844
BONYEZA HAPA ILI UWEZE KUCHAT NA MSHAURI WETU MOJA KWA MOJA WHATSAPP
0 Comments