Huwa Unasikiaga Watu Wakisema Kuhusu Chembe Ya Moyo???? Je Wewe Huwa Unaelewaga Nini??
Chembe moyo husababishwa na nini…?
Chembe moyo au kwa kitaalamu stable angina au angina pectoris. Ni aina ya maumivu ya kifua yanayatokea baada ya kupungua kwa mzunguko wa damu kwenye moyo. Kupungua kwa mzunguko wa damu husababisha kukosa hewa safi ya oksijeni kwenye moyo
Maumivu hutokea baada ya mwili kufanya kazi flani ama pale unapopata msongo wa mawazo
Maumivu haya ya chembe moyo husababisha mtu kukosa raha, kuhisi kama kifua kimejaa na kubana kwa kifua eneo la katikati.
.
.
Chembe Moyo Hutokea Wakati gani?
Chembe ya moyo hutokea pale misuli ya moyo inapohitaji damu ya kutosha zaidi kuliko kawaida. Mfano wakati unafanya mazoezi, au unapokuwa na msongo wa mawazo
Unapokua umetulia mfano umekaa kwenye kiti na kiwango cha hewa ya oksijeni kinachohitajika ni kidogo. Lakini unapokuwa kwenye shughuli kama kupanda mlima au kukimbia moyo unahitaji kiwango kikubwa cha hewa na ndio matokeo ya chembe moyo.
.
.
Dalili za Chembe Moyo:
Pamoja na maumivu na kubana kwa kifua dalili zingine za chembe ya moyo ni kama:
• Kushindwa kupumua vizuri
• Kupata kichefuchefu
• Mwili kukosa nguvu na kupata ganzi
• Kutokwa na jasho na
• Msongo wa mawazo
• Mazingira na tabia Hatarishi Zinazopelekea kupata Chembe moyo
• Kuwa na uzito mkubwa na kitambi
• Kuwa na historia ya kugua magonjwa ya moyo
• Kuwa na kiwango kikubwa cha cholesterol au shinikizo la damu kuwa juu
• Mgonjwa wa kisukari
• Uvutaji wa sigara
• Kutofanya mazoezi au kushugulisha mwili
• Kula mlo mkubwa
• Mazingira ya joto kali au baridi kali
.
.
Matibabu ya Mgonjwa wa Chembe moyo:
Matibabu kwa ajili ya chembe moyo yanahusisha, kubadili mtindo wa maisha, dawa na wakati mwingine upasuaji. Hakikisha unafatilia ni kipindi gani unapata maumivu, punguza mazoezi makali sana.
.
.
1.Mtindo wa maisha:
Mabadiliko ya mtindo wa maisha husaidia kupunguza hatari ya kupata chembe moyo. Mabadiliko haya yanahusisha kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara, kula lishe nzuri, na kuacha kuvuta sigara
Mabadiliko haya ya mtindo wa maisha yatakusaidia pia kuepuka magonjwa mengine kama kisukari, shinikizo kubwa la damu, na kuondoa cholesterol mbaya.
.
.
2.Dawa:
Daktari anaweza kukuanzishia dawa ili kupunguza maumivu ya chembe moyo. Pia kutokana na kisababishi chako cha chembe moyo kama shinikizo kubwa la damu, cholesterol au kisukari, daktari atakuanzishia dawa ili kutibu chanzo cha tatizo.
.
.
3.Upasuaji:
Upausaji (angioplasty) mara nyingi hutumika kwa wagonjwa wa chembe moyo. Upasuaji hulenga kutanua njia ya damu kweye mshipa ili kuruusu damu kupita.
.
.
Ushauri kwa Mgonjwa:
Wagonjwa wengi huchanganya chembe moyo kutokana na shida ya moyo, na maumivu ya kifua kutokana na gesi tumboni
Gesi ambayo inaweza kupanda mpaka juu kwenye kifua na kuleta maumivu makali sana. Hakikisha umepima na kujua chanzo cha maumivu yako ni moyo au mfumo wa chakula yaani gesi
Kama unapata dalili mbaya mara kwa mara, weka muda wa kwenda hospitali ufanye vipimo kujua chanzo cha tatizo lako
Kama tayari umefanya vipimo pamoja na dawa ulizopatiwa hospitali, nashauri tupigie simu upate dawa yetu iliyotengenezwa kwa mime ana mti ili kuondoa mafuta mabaya,kusafisha mishipa ya damu na kuimarisha mzunguko wa damu kuelekea kwenye moyo ili utibu chembe moyo
Endapo una tatizo hili au lolote lile la ki afya na ungependa upande suluhisho la kudumu basi usisite kuwasiliana nasi SASA HIVI.
Bonyeza neno WHATSAPP hapo chini ili uwezo kuchat na mshauri wetu na kuanza tiba
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
0 Comments