Games

6/recent/ticker-posts

Wanawake Wengi Hawajui Siku Zao Za Hatari Za Kudaka Ujauzito...HAYA NIMEKULETEA ELIMU YA BURE SOMA HAPA...

Zitambue Siku Hatari Za Kupata Mimba…

Kwa wastani,mzunguko wa hedhi ni siku 28

Mzunguko wa hedhi unaanza kuhesabiwa kuanzia siku ya kwanza mwanamke anapoanza ku bleed mpaka siku ya kwanza tena mwezi unaofuata anapopata tena bleed, jumla ya hizo siku ndio mzunguko wako. Sasa ukitaka kupata vizuri mzunguko wako fanya hivi :

Chukua kalenda yako, zungushia duara siku ya kwanza uliopata period, zungushia tena duara siku ya kwanza ya mwezi uliopata tena na uzungushie siku ya kwanza ya mwezi mwingine mpaka itimie miezi 3 halafu anza kuhesabu siku hizo. Utapata mwezi wa kwanza siku ngapi, mwezi wa pili siku ngapi na mwezi wa tatu siku ngapi

Mfano mwezi wa kwanza siku 28, mwezi wa pili siku 30 na mwezi wa tatu siku 25 baada ya hapo jumlisha yaani 28+30+25 =83 . Sasa kwakua ulichukua miezi 3 basi gawanya kwa 3 , ungechukua miezi 6 ungegawa kwa 6

Kwahiyo 83÷3 = 27.66  Kwahiyo mzunguko wako wewe ni siku 28 maana 27.6 ni sawa na 28 nadhani watu wa hesabu mnajua hapa . Kila mtu afuatilie miezi yake 3 aangalie yeye mzunguko wake ni upi.. piga hesabu halafu niambie kama umeweza kujua au bado

Mzunguko Wa Hedhi Wa Kawaida Una Sifa Madhubuti, Zijue…

1.IDADI YA SIKU KATIKA MZUNGUKO MMOJA

Kwa kawaida idadi ya siku katika mzunguko ambazo huhesabika kama ni mzunguko wa kawaida ni siku 21 hadi 35 (ambapo hapo ndipo unapata wastani wa siku 28 yaani [(21+35)÷2].

Kwahiyo ndugu msomaji usikariri kuwa mzunguko wa kila mwanamke una siku 28,hiyo ni big NO.wengine wana siku 27,wengine 25,wengine 35,wengine 29.. 

2.SIFA YA PILI NI UWIANO WA IDADI YA SIKU ZA MZUNGUKO KATI YA MZUNGUKO MMOJA NA MWINGINE

Hii ni miongoni mwa changamoto kubwa sana katika suala zima la ufanyaji wa tendo la ndoa kwani inaweza kuwa vigumu kuzitambua siku hatarishi kwa mwanamke kupata mimba.

Ili tuseme mwanamke anamizunguko ya hedhi iliyo sawa[regular cycles],idadi ya siku za mizunguko ya hedhi kati ya mwezi na mwezi isitofautiane kwa zaidi ya wiki moja ( siku 7 )

Kwa mfano,kama mwezi wa kwanza aliona siku zake baada ya siku 28,mwezi wapili akaona baada ya siku 30,mwezi wa tatu akaona baada ya siku 35 bado mzunguko wake uko kwenye uwiano mzuri[regular cycle] kwasababu mzunguko mmoja na mwingine haujatofautiana kwa zaidi ya siku 7.

Usikariri kuwa siku za mzunguko kwa kila mwanamke ni siku 28,hiyo ni big NO.Hiyo 28 ni wastani tu

Pia tambua ya kuwa si lazima idadi ya siku katika mzunguko mmoja ilingane na mzunguko mwingine kwa mwanamke huyohuyo

Kwa mfano usitarajie kuwa kama mwezi march ame bleed baada ya siku 28 na mwezi april pia ata bleed baada ya siku 28,sio lazima iwe hivyo lakini pia inaweza tokea.

Kwa mfano mwanamke mzunguko huu anaweza kuona siku zake baada ya siku 28,mzunguko unaofuata baada ya siku 27,mzunguko mwingine baada ya siku 30,mzunguko mwingine baada ya siku 29,mzunguko mwingine baada ya siku 25 na bado yuko kwenye uwiano sawa(tofauti si zaidi ya siku 7).

3.IDADI YA SIKU ZA KUBLEED[MENSTRUAL PERIOD]

Usichanganye kati ya menstrual period na menstrual cycle,hivi ni vitu viwili tofauti kabisa.

Siku ya kwanza ya kubleed ndo siku tunayoanza kuhesabu mzunguko wa hedhi[day one],sio siku ya kumaliza ku bleed. Kwa kawaida idadi ya siku za ku bleed ni kati ya siku 3 hadi 7,kila mwanamke ana idadi yake kati ya hizo

4. SIFA YA MWISHO YA MZUNGUKO WA HEDHI NI WINGI WA DAMU

Damu inayotoka wakati wa hedhi mwanamke anaweza ku bleed kawaida[normal bleeding] au ku bleed sana[heavy bleeding]

ILI KUZIFAHAMU VIZURI SIKU HATARI KWA MWANAMKE KUPATA MIMBA HEBU TUANGALIE KIDOGO JINSI MAYAI YANAVYOKOMAA NA KISHA KUTOLEWA KWENYE OVARY.

Mzunguko wa ovary[ovarian cycle) ndio unaoleta mabadiliko katika mfuko wa uzazi(menstrual cycle).

Mzunguko wa ovary una hatua zifuatazo

Follicular phase,ovulation na luteal phase.

1.FOLLICULAR PHASE

Sehemu hii ya mzunguko huanza siku ya kwanza ya mwanamke ku bleed mpaka yai linapokuwa limekomaa

Mayai ya mwanamke huanza kutengenezwa wakati akiwa tumboni mwa mama.

Mpaka kufikia kuvunja ungo,mwanamke anakuwa na mayai yapatayo 400,000 ndani ya ovary,mayai haya huwa katika hatua ya uchanga[primary oocyte].

2.OVULATION

Katika hatua hii ya mzunguko wa ovary,yai lililokomaa[graafian follicle] hutoka kwenye ovary na kuingia kwenye mirija ya fallopian.

SASA TUTAITAMBUAJE SIKU YA YAI KUTOKA ( OVULATION )???

Kiuhalisia ni ngumu kujua siku halisi yai lilipotolewa lakini tunaweza kuzitambua siku nyeti ambazo zitatupa nafasi kubwa ya kutokulikosa yai ndani ya siku hizo.Fuatilia hapo chini.

3.LUTEAL PHASE: hii ni sehemu ya mzunguko wa ovary ambayo huanza baada ya yai kutoka[ovulation] na kuishia kabla ya kuanza ku bleed[mwanzo wa mzunguko mwingine)

ZINGATIA HAPA

Idadi ya siku kati ya ovarian cycle na menstrual cycle ni sawa[mfano,28,30,35,25).

Idadi ya siku katika luteal phase ni sawa kwa mizunguko yote na ni siku 14.

ANGALIA HESABU HII RAHISI

Kwa mfano kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 28,kuipata siku ya ovulation tunachukua 28-14 tunapata 14,kwahiyo kutoka siku ya kwanza mwanamke alipoanza kubleed ni siku ya 14 ndipo yai linakuwa tayari kurutubishwa

Kwa mwenye mzunguko wa siku 30, tunachukua 30-14(luteal phase)=16,kwa hiyo mwanamke mwenye mzunguko wa siku 30,ovulation inauwezekano mkubwa wakutokea siku ya 16 na si ya 14(kuwa makini hapo).

Yule mwenye mzunguko wa siku 35,ovulation day ni 35-14 = 21,kwa hiyo kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 35,ovulation ina nafasi kubwa ya kutokea siku ya 21 na si ya 14.

Sasa baada ya kuijua siku ya ovulation lazima uwe makini na siku zinazokaribiana na siku ya ovulation kwani nazo ni siku hatari pia.

KWANINI?

Mbegu ya kiume inauwezo wa kuwa hai hadi masaa 48 (2 days) tangu shahawa zimwagwe na yai lina uwezo wa kuwa hai hadi masaa 24 tangu lilipotoka kwenye ovary.

Kwaiyo kama mwanaume akijamiiana na mwanamke siku mbili kabla ya yai kutolewa kwenye ovary, mbegu inaweza kuwa hai bado na kutungisha mimba endapo yai litatolewa ndani ya siku mbili zijazo kwa mfano kama siku ya ovulation ya mwanamke ni siku ya 14, mwanamke akijamiiana na mwanaume siku ya 12, uwezekano wa kupata mimba ni mkubwa

Kadhalika kama mwanamke ametoa yai siku ya 14 kisha akajamiiana ndani ya masaa 24 mbele, pia anaweza kupata mimba kwasababu kipindi mbegu zinamwagwa zinaweza kulikuta yai bado lipo hai na kutungisha mimba.

Kwa ufupi,ni siku tatu tu ndizo hatarishi sana kwa mwanamke kupata mimba,yaani,siku mbili kabla ya ovulation na ndani ya masaa 24 baada ya ovulation

Kwa kuongezea,kipindi cha ovulation mwanamke anapata nyege kali sana kwasababu ni kipindi ambacho kuna homoni fulani[androgens] ambazo huchochea nyege huzalishwa kwa wingi. Pia kipindi hicho cha ovulation au karibia ovulation joto la mwili la mwanamke hupanda,anajihisi mwili kuchemka tofauti kidogo na ilivyo kawaida yake.

SASA BASI KWA KUWA NIMESEMA HATUWEZI KUWA NA UHAKIKA WA 100% WA SIKU YA OVULATION NDO MAANA HUWA TUNATUMIA KANUNI YA KUEPUKA NGONO KWA KIPINDI CHA WIKI NZIMA[7 DAYS] AMBAZO NI SIKU ZILIZO KARIBU SANA NA SIKU YA OVULATION KWA WALE WANAOTUMIA CALENDER METHOD

Mfano,kama una mzunguko wa siku 30, kuipata siku ya ovulation chukua 30- 14=16,kwa hiyo siku ya ovulation ni ya 16 tangia ulipoanza kuona damu siku ya kwanza.sasa kama ni siku ya 16,ondoa siku nne kabla ya hiyo siku ya ovulation.kwahiyo kuanzia siku ya 12 hapo,acha ngono.

Pia jumlisha siku 3 mbele,ambapo mwanamke atatakiwa kuanza ngono kuanzia siku ya 19 huko ili kuepuka mimba 

USHAURI:

Ila kwa wana ndoa ambao wanahitaji mtoto hizo siku za hatari ndio mcheze nazo, kama wote mpo vizuri yaani hamna shida kwenye uzazi basi kwa uwezo wa ALLAH basi mwanamke atashika ujauzito. Endelea kujaribu kila mwezi siku hizo za hatari. 

Na pia endapo wanandoa watafanya tendo siku ile ya Ovulation au siku moja kabla au moja baada basi kuna uwezekano mkubwa sana kupata mtoto wa kiume. Ila hii usiiweke kichwani sana maana suala la jinsia ya mtoto ni MUNGU ndio anajua ila kisayansi ndio hesabu zinasema hivyo

Pia wanandoa hawa wanatakiwa kufanya tendo hili mara moja moja hasa wakati wa tarehe za hatari ili kuweza kubahatisha ujauzito. Hakikisheni hizi siku 7 ndio za kucheza kwa kujiachia zaidi na epukeni msongo wa mawazo na mawazo ya ujauzito

Wanawake wengi wanakosa kupata ujauzito kwa sababu ya kuuwazia sana ujauzito na ukitaka kuhakikisha hilo angalia wenye ndoa wengi wanaohitaji mtoto sana huchelewa kupata au wasipate ila wadada wa kazi wa ndani ukijaribu tu imetiki. 

Sababu kubwa wana ndoa wanawaza sana kupata watoto wakati wadada wa kazi hawana stress zozote zile, kwahiyo tambua msongo wa mawazo wa kutaka kudaka ujauzito ni hatari sana kwa mwanamke anayetaka kudaka ujauzito

Najua magubu ya mama mkwe, mawifi, majirani na wakati mwingine hata kwa mume mwenyewe yanafanya leo hii wanawake wengi kukosa ujauzito kwa haraka. Acha mwili u relax na ufanye tendo kama starehe tu utashangaa unaanza kutema mate.. kitu kishanasa

Inawezekana umejaribu sana kudaka ujauzito na umeshindwa basi kwanza lazima uchunguze sababu inaweza kuwa nini maana inaweza kuwa una shida kwenye homoni zako au kizazi,hujui siku zako hatari, mbegu za mwanaume ni chache na hazina uwezo wa kutungisha ujauzito au sababu zingine kadha wa kadha kwa wanandoa wote wawili basi usikae kinyonge jamani MUNGU atakupa hitaji la moyo wako

Afya yako ndio utajiri wako tumekuandalia package nzuri sana ya uzazi kiitwacho FERTILITY PACKAGE ambapo utatumia wewe na baba au wewe peke yako. Package hii imewasaidia wanawake wengi sana na tuna uhakika hata wewe utaweza kupata msaada huu na hatimae kuitwa mama siku za mbeleni. MUNGU hamuachi mja wake

Kwa ushauri zaidi au tiba wasiliana nasi kwa:

Simu/whatsapp: +255716778844

MUHIMU:

Hakikisha una follow hii page ili uwe wa kwanza kupata habari mpya kila tunapo post. Nenda chini kabisa ya post hii utakuta sehemu imeandikwa follow...

BONYEZA HAPA ILI UWEZE KUCHAT NA MSHAURI WETU MOJA KWA MOJA KWA NJIA YA WHATSAPP



Post a Comment

0 Comments