JE UMEKUA UNAJIULIZA KWANINI UNATOKWA NA HARUFU MBAYA SEHEMU YAKO NYETI ??? SOMA MPAKA MWISHO UPATE ELIMU
Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul
Ni matumaini yetu unaendelea vyema mpendwa msomaji wetu,leo tutajadili mada hiyo hapo juu ambayo ni miongoni mwa matatizo yanayotusumbua katika jamii tunayoishi
Tatizo la kutokwa na harufu mbaya ukeni ni moja ya matatizo yanayowasumbua wanawake wengi nchini na ni tatizo linalokera na gumu kuongeleka kutokana na wanawake wengi kuona aibu na kuhisi ni hali mbaya kwa mtu mwingine kuifahamu.
Kutunza uke na kulinda afya ya uke ni jambo la muhimu sana kwa mwanamke, kutokwa na harufu mbaya ukeni ni kiashiria kwamba unaumwa na hayuko sawa. Hali hii inaweza kuathiri heshima ya mwanamke na pia mahusiano na mwenza wake.
Harufu mbaya ukeni kwa kiasi kikubwa husababishwa na bacteria yaani tunaita bacteria vaginosis (BV) japo siyo kila mara ndio maana kuna umuhimu wa kutafuta chanzo cha tatizo la kunuka uke
Kama wewe muhanga wa tatizo hili basi tambua kwamba kuna njia za asili unaweza kuzitumia ikiwemo lishe ,virutubisholishe na ukarudi katika hali ya kawaida,kama tatizo litazidi kuendelea basi itatakiwa uende hospitali ili upate uchunguzi.
Ni kawaida kwa mwanamke kupata harufu ukeni kutokana na hali ya uke kujisafisha wenyewe kutoa vimelea wabaya. Lakini pale harufu inapokuwa kali sana mfano wa harufu ya shombo ya samaki basi ujue kuna tatizo kubwa.
Kutokwa na harufu mbaya ukeni huwa inaambatana na dalili zingine kama kuwasha na kuchomachoma na kutokwa na majimaji au uchafu kama mtindi ukeni.
VISABABISHI NA VYANZO VYA TATIZO LA KUTOA HARUFU MBAYA UKENI :
✳UKUAJI WA BACTERIA WA VAGINOSIS(BV)
Miongoni mwa sababu kuu ya kupata harufu mbaya ukeni ni ukuaji wa bacteria wa vaginosis,ukuaji wa bacteria usio wa kawaida kwenye uke husababishwa na kubadilika kwa mazingira ya ukeni na kushuka kwa kinga
Bacteria vaginosis ni chanzo namba moja kinachosababisha uke kutoa harufu mbaya.
Inawezekana ukawa msafi mpaka mwisho lakini ukisumbuliwa na hili tatizo basi lazima uke wako utatoa harufu mbaya.
Kila uke una bacteria ambao wapo naturally kwa ajili ya afya njema ya uke wako, nikiwa ba maana bakteria wanakua wale wabaya na wale wazuri Lakini kama ikitokea hawa Bacteria wabaya wakazidi na kuwa wengi kupita wale wazuri (walinzi) ndipo tatizo hili la BV hutokea
Madaktari wanasema BV inaweza ikasababishwa na kitendo cha kupeana Raha na Utamu bila condom na hasa kama vitu vilivyoingia kwenye uke wako wakati wa kupeana Raha na Utamu vilikuwa vichafu(mfano vidole au uume au dildo nk),lakini pia tatizo hili la ukuaji wa bacteria vaginosis hutokea kwa sababu mbalimbali ila pia linaweza kutokea bila sababu.
Ukitaka Kujua kuwa unasumbuliwa na bacterial vaginosis utajikuta unapata Dalili zifuatazo;
➡Uke kutoa maji maji mazito au mepesi yenye rangi ya njano au brown yenye harufu mbaya
➡Maumivu kwenye maeneo ya kiuno au nyonga
➡Unaweza usipate au ukapata maumivu ya kichwa
➡Uke wako unaweza ukawa unawashwa au usiwashwe
➡Pia Ukuaji wa bacteria wa vaginosis ndani ya uke wanaweza kupelekea mimba kutoka, kujifungua kabla ya wakati na kuongezeka kwa hatari ya kupata magonjwa mengine ya ngono.
Dalili mojawapo ya kwamba tayari una maambukizi ya bacteria ni kutokwa na uchafu unaoambatana na harufu kali mfano wa harufu ya samaki wabichi
✳UGONJWA WA TRICHOMONIASIS
Trichomoniasis ni moja ya ugonjwa wa ngono unaosababisha harufu kali ukeni.
Ugonjwa huu husababishwa vimelea na huambatana na kutokwa na uchafu ukeni,kuwasha, na maumivu makali wakati wa kukojoa.
Trichomoniasis inaweza kuwaathiri wajawazito na kuleta hatari ya mimba kutoka.
Kama utagundua una Trichomoniasisi basi wewe na mwenza wako mnatakiwa kutibiwa. Hakikisha pia unatumia condom vizuri kila unapofanya ngono kama kinga dhidi ya magonjwa
✳MABADILIKO YA HOMONI
Mabadiliko ya homoni kutokana na mzunguko wa hedhi huweza kuchangia harufu mbaya ukeni,wanawake wanaokaribia kukoma hedhi wako kwenye hatari zaidi kwani homoni ya estrogen hupungua sana hivyo kusababisha tishu kuwa na tindikali kidogo
✳YEASTS INFECTIONS(FANGAS)
Hili Pia ni Tatizo,lipo kama la Bacterial Vaginosis.tofauti yake ni kuwa kwenye Bacterial Vaginosis waliokuwa wamezidi ni bacteria lakini huku wanaozidi ni fungus candida albicans.
Ni wanawake wachache huwa wanapata Bacterial Vaginosis lakini wanawake wengi lazima wapate Yeast infection japo mara moja katika maisha yao.
Mara nyingi yeasts infection hutokea tu au inaweza kusababishwa na aina ya vyakula au vinywaji unavyokula au kunywa hasa kama vimejaa fangas(vyakula vyote vinavyotengenezwa na hamira,pombe etc)
Sababu nyingine kubwa ya hii fangas ni kupenda kula vyakula au vinywaji vyenye SUKARI kwa wingi. Na hii inawatokea sana wanawake maana wao wanapenda sana vitu vyenye sukari
Ukitaka kujua kama unasumbuliwa na yeast infection utajikuta unapata Dalili zifuatazo;
👉Uke wako ukawa unawashwa au usiwashwe
👉Maumivu kama uke unaungua pale unapokuwa unajisaidia haja ndogo
👉Uke kutoa maji maji mazito yenye rangi nyeupe kama jibini
✳KUTOZINGATIA USAFI
Ni wazi kwamba uchafu na kuwepo kwa unyevunyevu sehemu za siri huzalisha harufu mbaya. Kisayansi ni kwamba tezi zilizopo ndani ya mwili (apocrine sweat glands )hutengeneza mafuta kuelekea kwenye maeneo kama kwapa, pua, ndani ya sikio, uke, na kwenye chuchu, bacteria waliopo maeneo hayo huchakata mafuta haya na hivo kuzalisha harufu kali.
Uvaaji wa nguo zilizobana na uzito kupita kiasi huchangia kuhifadhiwa kwa jasho kwenye mikunjo ya ngozi na hivo kuleta harufu.
✳VAGINAL/CERVICAL CANCER(KANSA YA UKE/KANSA YA MLANGO WA KIZAZI)
Unapokuwa una kansa ya uke au kansa ya mlango wa kizazi ni kawaida kutokwa na maji maji yenye harufu mbaya ambayo ni sehemu ya dalili za kansa ya uke,.
Unapojiona kuwa una tatizo la uke kutoa harufu mbaya,ni heri na itakuwa busara ukienda hospitali,kupima na kama ni kansa ya mlango wa kizazi itakuwa sio ngumu kuitibu kama ukiwahi mapema kuanza matibabu
✳KUVAA PEDI MOJA MUDA MREFU
Pedi inapovaliwa kwa muda mrefu husababisha ngozi kucharuka,kututumka na kuwasha na pia kuchangiwa kukua kwa bacteria na fangasi wabaya ambao ni chanzo cha harufu..
MATIBABU
Matibabu ya tatizo hili hupatikana katika hospital zote nchini na matibabu hutolewa baada ya vipimo vya kitaalamu kuchukuliwa na daktar au nesi mwenye uzoefu wa kutosha juu ya magonjwa ya wanawake
MAMBO 6 UNAYOWEZA KUFANYA KUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA TATIZO LA KUTOKWA NA HARUFU MBAYA UKENI
➡Siku zote vaa nguo za ndani zisizobana sana na za pamba
Nguo zilizobana zinazuia kupita kwa hewa safi kuelekea ukeni na hivo kusababisha unyevunyevu ambao ni mbolea kwa bacteria na fangasi wanaoleta harufu mbaya kwenye uke.
Hakikisha unabadilisha chupi kila baada ya masaa 12 inasaidia kuzuia kukua kwa bacteria wabaya.
➡Badili Nguzo zako Kila Baada ya Kufanya Mazoezi
Nguo zenye unyevu ni mbolea nzuri kwa ukuaji wa bacteria hivo hakikisha unavaa nguo zilizokauka na kubadilisha kila baada ya kutoka mazoezini.
➡Punguza uzito kama Inawezekana
Uzito mkubwa unakufanya utokwe na jasho kwa wingi zaidi hasa kwenye uke. Na kama tulivojifunza pale juu, jasho na unyevunyevu inaleta fangasi na bacteria wabaya.
➡Epuka Kuflash Uke Kila Mara (Douching)
Kusafisha uke kila mara hasa kwa kutumia kemikali na sabuni inaharibu mazingira ya bacteria wazuri ambao ni walinzi, na hivo kuacha nafasi kwa uke kushambuliwa na bacteria wabaya pamoja na bacteria wa vaginosis
➡Epuka Kutumia Spray na Marashi ili Kuondoa Harufu Mbaya Ukeni au Kuweka Harufu Nzuri Ukeni.
Ukweli ni kwamba ngozi ya uke ni laini sana kwa hiyo inanyonya kwa urahisi kemikali zilizopo kwenye spray kuingia kwenye damu.
Usiingie kwenye mtego huu, kumbuka miili yetu imeumbwa kujisafisha yenyewe, Pale unapoongeza kitu cha ziada basi unaharibu normal flora na kuharibu kinga ya mwili.
➡Epuka Baadhi ya Vyakula Ambavyo ni Adui wa afya yako
Kuna aina nyingi ya vyakula ambavyo vinaweza kukuathiri wewe kama mwanamke kwenye swala la uzazi, vyakula hivi vinaharibu mazingira ya uke, kuua bacteria wzuri na kubadili PH.
Vyakula vyenye sukari, Pombe, ngano na vyakula vilivyosindikwa huchochea ukuaji wa bacteria wa vaginosis.
MAMBO YA KUFANYA ILI KUKATA HARUFU MBAYA UKENI
Harufu kali kwenye uke mara nyingi inagundulika zaidi baada ya kufanya ngono na pia kwenye hedhi. Kwahiyo badala ya kukimbilia spray na kujisafisha ukeni ili kuondoa harufu tumia njia zifuatazo kwa muda kabla hujamuona dactari wako ama kupata Dawa za kutumia
MBEGU ZA UWATU(FENUGREEK SEEDS)
Loweka kijiko kidogo cha mbegu za uwatu (fenugreek seeds) ndani ya maji glasi moja na uache kwa usiku mzima. Kesho yake asubuhi maji haya yaliyolowekwa mbegu za uwatu kabla ya kula au kunywa chochote.
Uwatu husaidia kuweka sawa homoni za mwili na kuweka sawa mzunguko wa hedhi.
BAKING SODA(MAGADI SODA)
Baking soda inaweza kutumika ili kubalansi pH kwenye mwili. Kumbuka mwanzo tulivosoma kuhusu madhara ya kubadilika kwa pH. Ukibalansi pH basi tatizo la harufu kali linakuwa limeisha. Unaweza kutumia pia baking soda kama body spray na ukaepuka kujaza sumu mwilini. Chukua nusu kikombe cha baking soda weka kwenye beseni kubwa la maji ya kuoga kisha kaa tulia kwa dakika 15 mpaka 20 kwenye maji. Baada ya hapo Jifute kwa taulo sehemu zote usiache unyevu kabla ya kuvaa nguo
MAZIWA MTINDI
Chukua mtindi ujazo wa kijiko kidogo cha chai kimoja au viwili na tumbukiza ndani ya uke wako na uache huko angalau masaa 3. Mtindi una bakteria wazuri wanaohitajika ukeni kuweka sawa usawa wa PH (alikalini na asidi) na hivyo kuondoa maambukizi
Pia unashauriwa kunywa maziwa mtindi mara mbili kwa siku kuongeza kinga ya mwili wako kwa ujumla dhidi ya magonjwa mbalimbali
MATUNDA NA MBOGAMBOGA
Matunda yenye uchachu mfano machungwa, mapera na strawberries yana Vitamn C kwa wingi sana ambayo huimarisha kinga ya mwili na kusaidia utoaji wa sumu mwilini.
Chakula kama Parachichi na mboga za kijani ina Vitamn B6 na madini ya potasium ambayo huongeza hamu ya tendo la ndoa na kujenga kuta za uke hivo kuzuia hatari ya kushambuliwa mara kwa mara
KITUNGUU SAUMU
Kitunguu saumu kinafahamika tokea miaka ya zamani kwa uwezo wake mkubwa wa kuimarisha kinga na kupambana na maambukiz ya bacteria na fangasi.
Unaweza kukata kata punje 3 - 6 za vitunguu saumu unameza na maji kwa siku ama ukatengeneza juice ya vitunguu saumu ukawa unakunywa asubuhi kabla ya kula chochote. ENDAPO una matatizo ya vidonda vya tumbo au presha ya kushuka basi usitumie tiba hii
KARANGA/ALIZETI NA MBEGU ZA MABOGA
Matumizi ya karanga na mbegu kwenye mlo wako wa kila siku huzuia kukauka kwa uke kwa sababu kuna Vitamin E kwa wingi. Unaweza kutafuna mbegu za maboga,karanga, na alizeti kila siku kuweza kujitibu na kujikinga dhidi ya tatizo hili
NB: Njia hizi zote nilizozitaji zinahitaji uzitumie kwa muda mrefu kidogo kama mwezi na kuendelea ili upate matokeo mazuri unayoyataka
Tumeona uke unatakiwa ulindwe hasa kwa kuweka PH yake katika hali yake ya kuweza kupambana na vimelea wote wabaya. Lakini pia tumeona Vit E ina umuhimu wa kupandisha kinga hivyo kumuepusha mwanamke kupambana na maradhi mbalimbali.
Ndio maana tumekuandalia kiosho chenye sifa ya kuweka PH ya uke vizuri na kupambana na vimelea wabaya. Pia tumewaandalia virutubisho vitakavyopandisha kinga ya mwili kwa haraka sana.
Endapo unahitaji Kiosho chetu au virutubisholishe vyetu vika ofisini kwetu makumbusho na kama upo mkoani basi tunaweza kukusafirishia na ukitaka kufanyiwa delivery pia tunafanya .
Endapo unahitaji ushauri au tiba wasiliana nasi kwa mawasiliano haya hapa chini
Simu/whatsapp: +255716778844
BONYEZA HAPA ILI UWEZE KUCHAT NA MSHAURI WETU MOJA KWA MOJA WHATSAPP
0 Comments