Je Unajua Sababu Za Mwanamke Kukosa Hedhi au Kutopata Hedhi katika mpangilio maalumu (Amenorrhoea)????
Nimekua nakutana na kesi nyingi sana kutoka kwa wanawake wakiniambia hawapati hedhi na ukiangalia hawajafikia muda wa kukoma hedhi... Haya hebu tufuatane kwenye hili somo..
AMENORRHEA Ni Nini??
Amenorrhea ni hali ya mwanamke ambaye amepevuka na kukomaa maumbile yake ya Uzaz kushindwa kupata hedhi/kupitiliza siku za hedhi
Kwa ufupi tatizo hili limekua likiwakumba na kuwaletea usumbufu wa kisaikolojia wanawake wengi wakidhani kwamba wamepata ujauzito nk, hata hivyo tatizo hili la kukosa hedhi linaweza kutokea awali au baadae kabisa maishani
KUNA AINA MBILI ZA AMENORRHEA
1.PRIMARY AMENORRHEA
Hii ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke/msichana aliye katika umri wa kuvunja ungo ambapo hali hii huweza kuendana na kutopata mabadiliko ya kimaumbile yanayoambatana na kuvunja ungo kama vile KUOTA NYWELE SEHEMU ZA SIRI, KUOTA MATITI, NK ila bado hapati siku zake
2.SECONDARY AMENORRHEA
Hii ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke ambaye si mjamzito wala hanyonyeshi na ambaye hajakoma hedhi na wala hatumii dawa za Uzazi wa mpango ambapo awali alikua akipata hedhi kama kawaida lakini akasimama kwa muda huenda ni miezi au mwaka mzima hapati hedhi mpaka sasa .
HEBU TUANGALIE KWANZA NAMNA AMBAVYO MWANAMKE HUPATA HEDHI
Kwa Kawaida ili mwanamke apate hedhi katika mzunguko ulio Sawa ni lazima tezi ya hypothalamus na pituitar pamoja na kiwanda cha mayai(ovaries) viwe vinafanya kazi kwa ushirkiano yani sawasawa .
VYANZO VYA TATIZO HILI .
👉Uvimbe katika ubongo karibu na tezi ya pituitar
👉Ukosefu au upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwa via vya Uzazi
👉Uzito mdogo kuliko Kawaida
👉Pituitar kushindwa kufanya Kazi vizuri baada ya seli zake kufa hii ni iwapo mama alipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua
👉Kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin katika damu (PROLACTINEMIA)
Proclatin ni homoni inayochochea uzalishaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha hivyo Hali ya kuwa proclatin nyingi katika damu husababisha kukosa hedhi
👉Msongo wa mawazo
👉Kuziba kwa utando unaozunguka uke (HYMEN) hivyo kukosekana tundu la kupitishia damu (IMPERFORATE HYMEN)
👉Mazoezi makali ya mwili na ulaji mdogo wa chakula, tabia hii hushusha homoni ambayo inahusika na kuweka siku zako katika Hali nzuri yaani hufanya leptin kuwa katika kiwango cha chini sana hivyo ni hatari
👉Baadhi ya magonjwa ya viungo vya Uzazi yamekua yakiambatana na kusimama kwa hedhi mfano wa magonjwa hayo ni POLYCYSTIC OVARIAN SYNDROME
👉MENOPAUSE ~hii ni hali ambayo hutokea kipindi cha miaka 42_55 homoni zinazohusika na kupata hedhi huwa Kwenye kiwango cha chini sana kiasi hufanya haziwezi kufanya kazi sawasawa
DALILI ZA TATIZO HILI :
👉Mwanamke kuwa na vinyweleo vingi na kuota ndevu hii inamaanisha na kuashiria kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni za kiume za ANDROGEN .
👉Kuongezeka uzito kupita kiasi
👉Matiti kutoa maziwa wakati mwanamke si mjamzito wala hanyonyeshi
👉Mwanamke kuwa na mhemko kuliko kawaida
👉Uke kuwa mkavu
👉Kutokwa jasho sana wakat wa usiku
👉Mabadiliko katika kupata usingizi vinaweza kuashiria kuwepo kwa tatizo katika ovaries
MATIBABU NA JINSI YA KUJIKINGA NA TATIZO HILI
Matibabu ya kukosa hedhi yanaweza kutibiwa hospital kutokana na chanzo cha tatizo ambapo huwa ni kupewa dawa au kufanyiwa upasuaji .
Pia waweza kufanya mambo yafuatayo ili kujiepusha na tatizo hili
👉Zingatia ulaji ulio sahihi ambao ubahisisha ulaji wa natunda kwa wingi na mboga za majani
👉Tumia maziwa ya soy au juice ya tikitimaji
Fanya masaji kwenye sehemu ya chini ya tumbo kwa kutumia maji ya uvuguvugu ukiwa kwenye siku zako (hedhi) sababu hii itasaidia kuongeza damu nyingi kutoka
Kula chakula kisichotokana na damu (Vegetarian diet) chenye protini nyingi mfano Nazi, Maharagwe, Korosho nk
MADHARA YANAYOWEZA KUTOKEA IWAPO TATIZO HILI HALITAPATIWA MATIBABU MAPEMA
👩Mwanamke kuchelewa kuingia menopause hali huu ni mbaya kwani huweza kusababisha SARATANI YA MATITI
👧Mwanamke kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa kwasababu ya kupungua kwa hamu ya kufanya mapenzi na uke kuwa mkavu
👧Husababisha matatzo ya kutopata usingizi
👧Matiti husinyaa
USHAURI
Tumekuandalia program nzuri ya kukusaidia kuondokana na tatizo hili Pamoja na matatizo mbalimbali kwa kutumia virutubisho lishe
Tib hii ina mchanganyiko wa miti na mimea mbalimbali iliyotengenezwa kwa teknolojia nzuri Kwahiyo utakapotumia itakusaidia kuondoa shida hii kwa kurekebisha homoni zako ambazo ndio zinazohusika na wewe kupata hedhi na mfumo mzima wa uzazi wako
Ukishaanza kupata hedhi yako ina maana uwezekano wa wewe kupata ujauzito kama ulikua ndio unauombea kila siku basi ujue utakua ni mama mtarajiwa siku za usoni. Najua watoto ni baraka, watoto ni heshima na watoto ni furaha.. Wewe pia utaitwa MAMA kijacho siku zi nyingi
Endapo unahitaji msaada, ushauri au program hii basi tuwasiliane kwa:
Simu/whatsapp: +255716778844
BONYEZA HAPA ILI UWEZE KUCHAT NA MSHAURI WETU MOJA KWA MOJA WHATSAPP
0 Comments