Kosa kubwa moja ( 1 ) wanalofanya wanaume wengi pale wake zao wanapochelewa kushika ujauzito
Nipende kutumia nafasi hii kutoa pole kwenye ndoa yoyote ambayo wamekuwa wakipitia changamoto ya kutopata mtoto kwa kipindi kirefu.
Ninafahamu ni kwa jinsi gani tatizo hili linavyosumbua kwenye nyumba nyingi hasa miaka ya karibuni.
Wapo waliohangaika mpaka wamekata tamaa
Wameshatumia pesa nyingi, wameshatumia dawa nyingi lakini bado hakuna majibu.
Wengine wamekuwa ni watu wa mawazo tu muda mwingi na hawana amani kabisa moyoni.
Hakuna furaha kwa mtu yoyote hata kama ni tajiri kama hana mtoto
Kila mtu yupo bize anahangaika na maisha kwa ajili ya mambo mengi lakini namba moja huwa ni kwa ajili ya watoto wake.
Utamuona baba anaamka mapema saa kumi na moja anaoga na kuelekea kazini au kwenye mihangaiko mingine kwa ajili ya watoto wake
Kwahiyo nafahamu ni madhira gani wanapitia wanandoa ambao hawafanikiwi kupata mtoto kwa kipindi kirefu.
Wengine wanaishi na stress, wengine wanatishiana kuachana, wengine wameishiwa hata hamu yenyewe ya tendo la ndoa na wanaweza kukaa hata wiki 3 hawajagusana.
Hali huwa mbaya zaidi mwanamke anapofikisha miaka 35 au 40 na bado hajapata mtoto
Kwa kifupi tu niseme siyo jambo rahisi kuishi na tatizo hili hasa ukizingatia maneno maneno ya ndugu, jamaa, marafiki na majirani juu yenu
Sasa kosa kubwa 1 wanalofanya wanaume wengi pale wake zao wanaposhindwa kupata ujauzito ni kuweka majukumu yote kuhusu tatizo hilo kwa wake zao pekee
Yaani mwanaume anafikiri sababu kubwa ya wao kutopata mtoto ni mwanamke na yeye mwanaume haimhusu
Jumba bovu lote anaangushiwa mke!
Ni mke ndiyo atapelekwa kufanya vipimo kisha majibu yanasema ni uvimbe kwenye kizazi au homoni zimevurugika au mayai hayapevuki, au ana chango la uzazi na kadharika, orodha haiishi
Atapatiwa dawa moja baada ya nyingine na hapo mwaka unaweza kupita, miaka miwili hata mitatu hata miaka mitano inaweza kupita bado wapo bize kuhangaika na matatizo ya uzazi kwa mwanamke peke yake!
Hapo mwanaume hana hata wazo la kufanya vipimo kujua ikiwa na yeye huenda ni sehemu ya tatizo
Na wapo wanaume kabisa ambao hukataa wazi wazi kufanya vipimo hata baada ya daktari kushauri mmeo naye afanye vipimo
Wanakataa kupima hata baada ya wake zao kuwaomba na wao kupima
Na baadhi ya wanaume ninao chat nao WhatsApp wana kisingizio cha kwamba wana watoto wa miaka miwili au mitatu au miaka kumi kabla ya kuoana na mke wa sasa
Mwanaume kama alipata mtoto sehemu nyingine miaka miwili nyuma moja kwa moja anajiona ni mzima na hana tatizo la uzazi
Hivyo mwenye tatizo atakuwa ni mkewe tu
Hapo ndipo mnapokosea sana
Kama ulipata mtoto miaka miwili nyuma au hata miezi 6 nyuma, haina maana hutapata tatizo fulani kwenye mfumo wako wa uzazi linaloweza kuwa ndiyo chanzo cha mkeo wa sasa kutopata ujauzito. Na kingine ni kwamba kuna watoto ambao unaambiwa wako kumbe sio wako.. ( watoto wa mchongo / umebambikiwa ) japo kisheria kitanda hakizai haramu...
Narudia tena : Kama wewe mwanaume unaye mtoto kabla ya kuoana na huyu mke wa sasa ambaye hapati ujauzito haina maana tatizo lote lipo kwa mwanamke huyo uliyenaye sasa Lah hasha tatizo linaweza kuwa hata kwako pia hivyo ni vyema mkaenda wote kucheki mifumo yenu ya uzazi
Unaweza kutungisha ujauzito mwezi huu na mwezi ujao ukapata tatizo la kuwa na mbegu chache, mbegu zisizokomaa vizuri, wingi wake unaweza kupungua pia na kadhalika
Wakati wowote unaweza kupata tatizo la kushindwa kutungisha ujauzito.
Hata kwa wanawake ipo hivyo kwamba anaweza kupata mtoto wa kwanza, wa pili na wa tatu vizuri tu lakini baadaye ikawa shida kupata ujauzito wa nne mpaka apate dawa ndiyo anapata ujauzito
Hili mbona unalifahamu lakini unashindwa kulieguza upande wako?
Wanawake wengi wanashikwa na mshangao kuona waume zao hawana habari ya kupima na majukumu yote wanapewa wao
Nimeshawaona wanawake wenye uvimbe kwenye kizazi au tumboni na bado kwa neema ya Mungu wanapata ujauzito.
Kumbe kwenye familia nyingine ikitokea mama amepima na amekutwa na uvimbe basi jukumu lote anaachiwa yeye.
Mpaka apone uvimbe mke ndiyo wanaamini watapata ujauzito
Unakuta Mungu anamsaidia huyu dada kweli uvimbe huo anapona lakini bado hawapati ujauzito
Daktari akimpima anarudisha majibu hana uvimbe na hana tatizo lolote linalozuia asipate ujauzito
Lakini bado mpaka hapo mume hana habari ya kupima na pengine anahamishia mawazo kwamba huenda ndugu yao fulani anawaloga, kumbe hakuna uchawi wowote zaidi ya uvivu wake au woga wake wa kuchukua vipimo
Ninaweza kuendelea kuandika na kuandika mengi sana kuhusu jambo hili lakini hoja yangu kuu ni kuwa inapotokea ndani ya nyumba yenu mnashindwa kupata mtoto, mwanaume usiache jukumu lote liwe kwa mwanamke
Na wewe shiriki vipimo na uwe sehemu ya suluhisho
Tena uzuri mwingine ni kuwa vipimo kwa wanaume huwa ni bei ndogo sana ukinilinganisha na gharama za vipimo hivyo hivyo kwa mwanamke
Na ikitokea kuna tatizo fulani kwenye mbegu zako linaloleta shida usitungishe ujauzito niachie tu ujumbe WhatsApp 0716778844 . FERTILITY PACKAGE kutoka Afya Yako Ndio Utajiri Wako imekua tiba pendwa sana kwa ajili kuimarisha mbegu za kiume na kusaidia kupevuka kwa mayai ya mwanamke hivyo kusaidia upatikanaji wa ujauzito na kufanya wanandoa kurudisha furaha yao
NB: Endapo wanandoa wamekua wakitafuta mtoto kwa muda mrefu bila mafanikio yoyote basi nashauri kwanza wote wawili kuhudhuria hospitali kwa ajili ya kuchunguzwa mifumo yao ya uzazi baada ya hapo wataweza kuendelea na tiba za hospitali na huku wakitumia package yetu ya FERTILITY PACKAGE ambayo imekua msaada sana kwa wanandoa wengi wanaotafuta watoto
Tafadhali mwanaume toa ushirikiano kwa mkeo pale inapotokea mmeishi muda mrefu bila kufanikiwa kupata mtoto
Pia kwa wale wanandoa wapya au wale mliopo kwenye ndoa changa nawaomba kujifunza kuwa na subira
Siyo mnaoana leo miezi mitatu tu baadaye tayari mpo bize mmeanza kujiuliza mbona ujauzito hautokei!!
Hamkuoana kwa ajili ya ujauzito tu...
Miezi 6 tu tayari watu wameanza kuuliza dawa ya kupata ujauzito.
Mna haraka ya wapi?
Jaribuni kuishi kwanza hata miaka miwili ya mwanzo bila kuwa na presha yoyote ya kuwa na mtoto
Na hata muda unapopita sana bila mafanikio bado hamhitaji kuwa na presha yoyote, na presha au stress inaongeza tu tatizo na kulifanya gumu kutibika.Hivi unajua mwanamke anapokuwa na mawazo sana ya kunasa ujauzito anaweza asinase kabisa???
Relax, tulia, cheza siku za hatari, omba Mungu, tumia dawa lakini bado endelea kumshukuru Mungu kwa uzima ulionao hadi sasa
Kwa ushauri , tiba au msaada zaidi wasiliana nasi kwa:
Simu/whatsapp: +255716778844
MUHIMU:
Hakikisha una follow hii page ili uwe wa kwanza kupata habari mpya kila tunapo post. Nenda chini kabisa ya post hii utakuta sehemu imeandikwa follow...
BONYEZA HAPA ILI UWEZE KUCHAT NA MSHAURI WETU MOJA KWA MOJA WHATSAPP
0 Comments