Games

6/recent/ticker-posts

ONYO: Kama Unapenda Kula Nyama Au Unafuga Mifugo Basi Soma Hapa Kwanza...

Wapenda kula nyama nyekundu na wafugaji kuweni makini


BRUCELLA NI NINI ???

Ugonjwa wa Brucella ni ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama Brucellosis na chanzo chake kikubwa ni maambukizi ya Bacteria wanaojulikana kama BRUCELLA

Bacteria hawa hutoka kwa wanyama mbali mbali kama vile; Ng'ombe, mbuzi,kondoo,Nguruwe,Mbwa n.k, na kwa hivi sasa watu wengi hupatwa na ugonjwa wa Brucella ambao hupimwa kupitia kipimo cha damu

DALILI ZA UGONJWA WA BRUCELLA

Fahamu kuhusu dalili mbali mbali za ugonjwa wa Brucella, kwa kusoma baadhi ya dalili hizo hapa chini;

1. Mgonjwa kupatwa na homa ambazo hujirudia mara kwa mara

2. Mgonjwa kuhisi kama vile kuna vitu vinatembea mwilini mwake, na wakati mwingine huhisi kama minyoo wakati wa kujisaidia haja kubwa

3. Mgonjwa kuanza kutetemeka mwili baada ya kuhisi baridi kali

4. Mgonjwa kupoteza kabisa hamu ya kula chakula au kitu chochote

5. Mgonjwa kutoa jasho kupita kiasi

6. Mwili kuchoka sana pamoja na kuwa dhaifu

7. Mgonjwa Kupata maumivu ya joints,misuli pamoja na maumivu ya mgongo

8. Mgonjwa Kupata maumivu ya kichwa mara kwa mara

9. Pia mgonjwa huweza kupatwa na tatizo la kuvimba kwa kuta za ndani ya chemba za moyo yaani endocarditis

10. Mgonjwa kupatwa na tatizo la kuvimba kwa joints pamoja na mifupa ya uti wa mgongo yaani spinal bones, tatizo ambalo hujulikana kwa kitaalam kama Spondylitis


YAFUATAYO NI BAADHI YA MADHARA ENDAPO MGONJWA HATOPATA TIBA KWA WAKATI :

👉Makovu au uharibifu wa mifupa na viungo
👉Kuvimba kwa ubongo
👉Kuvimba kwa sehemu ya ndani ya ubongo
👉Ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo

WATU GANI WAPO HATARINI ZAIDI KUPATA UGONJWA HUU ??

👉Watu wanaofanya kazi zinazohuisha kukutana na wanyama au nyama kama vile wachinjaji mifugo kule machinjioni , wakulima au wataalam wa wanyama 

👉Watu wanaokula nyama mbichi, ambazo hazijaiva vya kutosha

👉Watu wanaokunywa jibini au maziwa yaliyotoka kwa wanyama hao ambao wana ugonjwa huo


JINSI YA KUJIEPUSHA NA UGONJWA HUU

👉Hakikisha unachemsha maziwa vizuri kabla ya kunywa. Epuka kunywa maziwa mabichi

👉Hakikisha unapika nyama mpaka ziive vya kutosha badala ya kukimbilia kudokoa kabla haijaiva ahaah ahaha

USHAURI

Endapo umeanza kuona hizo dalili nilizozitaja basi harakisha kituo cha afya ili uangaliwe kama una huo ugonjwa na uanze matibabu mapema. Sisi kama Afya Yako Ndio Utajiri Wako tumekuandalia tiba nzuri ya virutubisholishe ambayo utaweza kutumia hata kama una dawa za hospitali umepewa ili uweze kupona kwa haraka sana

Karibu sana uweze kupata ushauri na tiba sasa kwa kuwasiliana nasi :

Simu/whatsapp: +255716778844

BONYEZA HAPA ILI UWEZE KUCHAT NA MSHAURI WETU MOJA KWA MOJA WHATSAPP







Post a Comment

0 Comments